November 26, 2016Bondia nyota wa ngumu za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’ amepata pambano nchini India.

Cheka amesema anakwenda kupigana India huku akikiri kwamba, njaa nayo ni tatizo.

Amesema atakwenda nchini India kucheza pambano la ubingwa wa WBC Asia Pacific dhidi ya Vijender Singh raia wa nchi hiyo kwani amechoshwa na njaa ya kukosa mapambano ya kucheza muda mrefu.

Pambano hilo la raundi 12 linatarajiwa kupigwa Desemba 17, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Michezo wa Thyagaraj Complex, Delhi, India.

 Cheka amesema: “Unajua kazi yangu ni ngumi na nina njaa ya mapambano kwa sababu nimechoshwa kukaa muda mrefu bila ya kucheza sasa, nitahakikisha napata ushindi.”


Hata hivyo, awali alisema anaamini India ni nchi inayokua haraka kimichezo, hivyo anaweza kupata ushindani mkali kuliko wengi wanavyotarajia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV