November 6, 2016

CHIEF CHUMA AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUZINDULIWA KWA MOJA YA MATAWI MAWILI ALIYOZINDUA MKOANI MBEYA, LEO

Klabu ya Yanga imeendelea kujitanua Nyanda za Juu Kusini baada ya kufungua matawi mapya.
Yanga ambayo ni klabu kongwe imezindua matawi yake katika maeneo ya Chimala lililopo Wilaya ya Mbalali na lingine la Kampa Kampa tena lililopo katika Wilaya ya Mbalizi, yote mawili mkoani hapa.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Omari Chuma maarufu kama Chief ndiye aliongoza zoezi hilo ambalo ni sehemu ya Yanga kuendelea kujitanua zaidi.
Chuma amesema kwamba, lengo la kamati yao ya Mashindano ya Yanga ni kuwaunganisha wanachama wake wote pia na kuhakikisha inaongeza idadi na molari kwa kila Mkoa ambapo timu hiyo itacheza.


“Niwashukuru sana wenye viti wa matawi haya ya Chimala na Kampa Kampatena kwa kunipatia fursa ya kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa matawi yao, nimehamasika kuja kuzindua kwa sababu lengo ni kuifanya Yanga iwe na wanachama wengi na pia uwe na nguvu kubwa kwa kila Mkoa.


“Sisi kamati ya Mashindano ya Yanga, mbali na kuhakikisha tunashinda kila mchezo, lengo letu jingine ni kuongeza idadi na hamasa kwa mashabiki wetu wa kila sehemu, kwani najua kufanya hivi ni kuiweka tumu yetu pamoja na kuifanya iwe na kauli moja kwa kila jambo tunalolihitaji,” alisema Omari Chuma.


Kwenye uzinduzi wa matawi hayo, Chuma alitoa jumla ya shilingi laki mbili ambapo kwenyeTawi la Chimala lilolpo Wilaya ya Mbalali alitoa shilingi laki moja kama moja ya mchango wa kuendeleza tawi hilo, wakati huohuo akatoa tena kiasi hicho katika tawi la Kampa Kampatena lililopo Wilaya ya Mbalizi Mkoani Mbeya.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic