November 24, 2016


Tanzania imeporomoka katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutoka nafasi ya 144 hadi ya 160.

Tanzania chini ya TFF ya Jamal Malinzi imekuwa ikiporomoka haraka hadi kufikia 160 sasa.
Hali hiyo inaonyesha wazi Tanzania imekuwa ikifanya mambo mengi kwa zimamoto bila ya kuangalia nini kinatakiwa.

Tanzania haina mipango bora ya maendeleo, hasa zile programu za muda mfupi na mitano.

Siasa pia imekuwa tatizo kubwa ndani ya mchezo wa soka, jambo ambalo linaonekana kuwa ni tatizo kubwa sana.

Timu ya taifa, sasa imerejea katika zile zama za Kichwa cha Mwendawazimu kwa kuwa kufungwa ni jambo la kawaida iwe mechi za mashindano au za kirafiki.

Hofu kuu ya kuendelea kuporomoka inatokana na kwamba, kwa sasa uongozi wa TFF umejikita zaidi kwenye kampeni za chinichini za uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Kama TFF chini ya Malinzi itaendelea na mipango yake ya sasa, hakuna ubishi kwamba itazidi kuporomoka kwa kasi kubwa na huenda hadi mwakani inaweza ikawa katika nafasi ya 190.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV