November 20, 2016Alichopendekeza Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog katika ripoti yake ni usajili wa wachezaji watatu pekee.

Wachezaji ambao amewataka Omog ni kipa, beki wa kati na mshambuliaji wa kati pekee.

Lakini taarifa za ndani kutoka katika kikosi cha Simba, Omog ameepuka kuwataja wachezaji wapi wasajiliwe na kusisitiza kiwango tu.
“Omog hajataja jina hasa la mchezaji, badala yake alilenga zaidi katika nafasi hizo tatu,” kilieleza chanzo.

Omog ameonyesha weledi, hajataka kulenga majina zaidi, badala yake nafasi na amesisitiza kikosi chake kutopanguliwa.

Ameona katika nafasi ya mabeki licha ya kuwa na mabeki watatu, lakini anaona anatakiwa kuongezwa mmoja ambaye ni imara.

Kwa upande wa kipa, bado anamkubali Vicent Angban lakini anaamini anastahili kupewa changamoto kutoka kwa kipa mwingine bora zaidi.

Kwa upande wa mshambuliaji wa kati, Omog ameonyesha anaamini washambuliaji Frederic Blagnon na Laudit Mavugo wanaweza kubadilika na kufanya vema.

Lakini anataka mtu ambaye atakuwa na kazi ya kutupia tu wavuni mabao bila ya kufanya mchezo kwa kuwa mzunguko wa pili utakuwa mgumu.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV