November 20, 2016


Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amesema angependa kurejea Tanzania na kufanya kazi tena.

Loga ambaye sasa anainoa Inter ya nchini Angola, amesema anaamini akiwa Tanzania ana nafasi ya kubeba kombe.

“Awali niliona hata Simba hawakunielewa, utaona kuna mengi niliwashauri wakati ule wakaniona sifai.

“Lakini leo kila ambacho hawakukikubali, ndiyo wanakifanya. Hii inanipa faraja kwamba mambo yanaweza kuwa mazuri.

“Ningekuwa na timu kama waliyonayo Simba msimu huu, ninaamini ningeweza kutangaza ubingwa mapema.

“Niko tayari kurudi Simba au timu nyingine yoyote ambayo itakuwa makini na tayari kupambana kwa ajili ya kutwaa ubingwa,” alisema.

Loga aliwahi kuwaeleza viongozi wa Simba kwamba alitaka timu ya wachezaji waliokuwa kikazi na si wale vijana.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV