November 28, 2016Uongozi wa timu ya Kagera Sugar, umesema kuwa unajipanga kuvuka boda na kwenda nchini Uganda kusaka mlinda mlango mzoefu atakayeisaidia timu hiyo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Kagera ambayo kwa sasa ina makipa watatu, Hussein Shariff ‘Casillas’, David Burhani na John Mwenda, inataka kusajili kipa baada ya kumsimamisha Casillas ambaye anatuhumiwa kuihujumu timu kwenye mchezo wao waliopoteza kwa mabao 6-2 dhidi ya Yanga.

Mratibu wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein, amesema, mpaka sasa wapo kwenye mchakato huo ambapo wameangalia hapa nchini lakini bado hawajaona, hivyo wana mpango wa kwenda Uganda kukamilisha azma yao hiyo.

“Kwa hapa Bongo, mpaka sasa bado hatujaona kipa wa kumsajili, lakini kama hali ikienda hivi, basi hatuna budi ya kuvuka boda na kwenda Uganda kuchukua kipa, tunataka tumpate mzoefu ambaye atakuja kutusaidia kwenye mzunguko wa pili wa ligi.


“Lakini kama mipango hiyo yote ikikwama, tutaangalia katika kikosi chetu cha vijana kipa gani atatufaa, basi tutampandisha aje kutusaidia kwa siku zijazo."

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV