November 6, 2016

MPIRA UMEKWISHAAA
-SUB: Matheo Anthony anaingia kuchukua nafasi ya Chirwa lakini ajabu wachezaji wa Prisons wanamfuata na kumsukuma hapa mbele ya mwamuzi
-Mwinyi anaachia mkwaju mkali hapa lakini hakulenga, goal kick
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
Dk 90 sasa, Prisons wanaonekana kutembeza kukata tamaa na sasa wanatembeza viatu tu
 Dk 86, Kimenya anapiga mpira wa faulo hapa lakini goal kick
Dk 84, Prisons wanaoenakana kushambulia mfululizo lakini bado

Dk 80, Niyonzima anaachua mkwaju mkali kwelikweli akiunganisha pasi ya Msuva lakini ni goal kick
GOOOOOOOO Dk 74, Msuva anaindikia Yanga bao kwa mkwaju wa penalti baada ya madhambi kufanyika eneo la 18 kwa Nurdin Chona kumuagusha Chirwa, Yanga moja
Dk 71, Mwasote wa Prisons anautoa mpira nje na kuwa kona, inachongwa na mabeki Prisons wanaokoa na kuwa kona nyingine, inachongwa na Niyozima, unaokolewa tena
Dk 67, Yanga wanapata kona hapa lakini mpira unaokolewa na kuwa wa kurusha. Bado ngome zote ni ngumu

Dk 63, Yanga wanafanya shambulizi tena, lakini bado inaonekana kuna ugumu wa kuipenya ngome ya Prisons
Dk 62, Ntala anafanya kazi ya zida, anatoka na kuuwahi mpira miguuni mwa Ngoma
SUB Dk 58, Tambwe anaingia kuchukua nafasi ya Deus Kaseke ambaye alisababisha mkwaju wa penalti ingawa wachezaji wa Yanga walipinga kuwa Hangaya alijiangusha
ANAOKOAAA Dk 55 Sabayanka anakwenda kupiga, Kakolanya anaokoa vizuri mkwaju huo na Yanga wakaokoa PENAAAAT Dk 53, Prisons wanapata penalt baada ya Hangaya kuangushwa na Kaseke
Dk 52 sasa, Yanga wanahjitahidi kutengeneza nafasi zaidi 
Dk 48, Hangaya aanaachia mkwaju mkali hapa, Kakolanya anadaka unamtoka lakini anauwahi tena
SUB Dk 46 Yanga inamtoa Yusuf Mhilu na kumuingiza Simon MsuvaMAPUMZIKO

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 44, Kimenya anaingia vizuri kutokea pembeni lakini Haji Mwinyi anafanya kazi ya ziada na kuokoa
Dk 42, Ntala analala na kudaka mpira wa krosi wa Niyonzima ambaye aligongeana vizuri na Ngoma
Dk 35, Kaseke anaachia shuti kali kwelikweli, lakini hakulenga lango. Goal kick
Dk 35, Kakolanya analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira ambao mabeki wake walikuwa wamejichanganya
KADI Dk 31, Twite analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Benjamini Asukile

Dk 27 sasa, bado hakuna mpira wa kuvutia sana, inaonekana kila timu inacheza kwa woga kuhofia kupoteza mechi kwa kuwa zote mbili zimepoteza mechi zao zilizopita
Dk 15, Prisons wanaingia vizuri lakini Hangaya anamuangusha Bossou, mwamuzi anasema ni faulo irudi Prisons
Dk 8, Kipa Ntala anaokoa anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Kamusoko
Dk 4, Bossou anarudisha mpira kwa Kakolanya, unakuwa mkubwa na kusababisha hatari lakini kipa huyo anajitahidi kuokoa
Dk 1, Mechi imeanza kwa kasi, Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Prisons lakini Asukile anauokoa mpira huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV