November 9, 2016



Huku wengi waliamini Kocha George Lwandamina anatua usiku wa maneno, yeye amesema anatua leo jioni.

LWanzamina raia wa Zambia, amezungumza na SALEHJEMBE na kusema anatarajia kutua leo jioni na kumalizana na Yanga.

"Sasa niseme kweli kwamba nakuja Tanzania. Natarajia kufika leo jioni ingawa nisikuhakikishie sana," alisema alipozungumza na SALEHJEMBE.

Awali ilielezwa alishanondoka Zambia kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam lakini amesema kulikuwa na mabadiliko.

"Kulikuwa na mabadiliko kidogo, lakini sasa naona safari yangu itaanza leo na jioni naweza kufika Dar es Salaam," alisema.

Huku Lwandamina anatarajia kutua, Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm amewaaga wachezaji wake jana.

Kocha huyo mwenye uzoefu na soka la Afrika, msimu uliokwisha hivi karibuni aliifikisha Zesco hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hali ambayo inawafanya Yanga kuamini kwamba akiwa hapo ataipa mafanikio makubwa zaidi ya yale waliyoyapata wakiwa na Pluijm msimu uliopita kwa kuchukua Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, huku wakifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Hata hivyo, chanzo makini kilichopo ndani ya timu hiyo ya Zambia kimethibitisha juu ya kuondoka kwa kocha huyo ambaye pia aliifundisha timu ya taifa hilo, Chipolopolo na kusema kuwa ameacha majonzi kwa kila mchezaji kwenye timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic