November 27, 2016

MOHAMMED DEWJI

Ile ishu ya bilionea shabiki wa Simba, Mohammed Dewji kumwaga mamilioni ya fedha kusaidia usajili wa kuwabakiza wachezaji Ibrahim Ajibu, Jonas Mkude na Mohamed Zimbwe, umeonekana kuwa faraja kwa mashabiki wengi wa Simba.

Badaa ya kuripotiwa jana, mashabiki wengi wamekuwa wakianzisha mjadala mitandaoni kwamba, wana imani wachezaji hao watabaki Msimbazi.

Tayari Simba imefanikiwa kumsainisha Zimbwe Jr maarufu kama Tshabalala mkataba wa miaka miwili.


Lakini mashabiki wengi walikuwa na hofu ya kuwakosa Ajibu na Mkude ambao tayari walionyesha wako tayari kwenda hata Yanga.


Hata hivyo kumekuwa na taarifa kuwa Ajibu, amekataa kusaini hadi mkataba wake utakapoisha ili aende akacheze nje ya Tanzania.


Lakini katika mijadala hiyo ya mitandaoni, wengi wanasema Ajibu alikuwa ‘anatikisa kiberiti’ kwa kuwa anataka kupata fungu la kutosha.


Taarifa nyingine zimeeleza, kamati ya usajili ya Simba, tayari imeanza mazungumzo na Ajibu na Mkude ili kufikia mwafaka ili waongeze mkataba kabla ya mwisho wa msimu na ikiwezekana kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV