November 27, 2016


Badaa ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland, jana. Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amewataka mashabiki wao kuendelea kuwaunga mkono lakini si kuweka mawazo ya ubingwa wa England.

Klopp raia wa Ujerumani amesema sasa ni mapema sana kuanza kuihesabia Liverpool kuhusiana na ubingwa kwa kuwa Ligi Kuu ya England haitabiriki.


“Kikubwa wandelee kutuunga mkono, lakini kingine wahakikishe wanaondoa mawazo ya ubingwa. Sasa si wakati wake kwa kuwa ligi hii ni ngumu sana,” alisema akihojiwa na Sky Sports.


“Sisi tuna kazi kubwa ya kuendeleza tunachokifanya, hivyo watuunge mkono na kama itafikia suala la kuanza kufikiria ubingwa. Kila kitu kitakuwa wazi, hata wao wataona,” alisisitiza.

Liverpool ipo katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 30 sawa na Man City iliyo katika nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Chelsea wenye pointi 31.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV