November 27, 2016Kauli ya Kocha mpya, George Lwandamina imewashitua wachezaji wa Yanga na wengi wao wameanza kujifua kimyakimya.

Mmoja wa wachezaji wa Yanga amesema pamoja na kuwa mapumziko, wamekuwa wakiendelea na mazoezi kwa kuwa walisikia kocha huyo kuwa likizo ya wiki mbili ni ndefu sana.

"Tumekuwa tunafanya mazoezi, nimewasiliana na (anataja wachezaji wanne), wote wanafanya mazoezi kabisa.

"Unajua baada ya kusikia anasema anaona likizo ni ndefu, kila mmoja amejiongeza. Hata wale walio nje nao wamekuwa wakisema wanajifua," alisema mchezaji huyo ambaye ni tegemeo katika kikosi cha Yanga.

Lwandamina amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm ambaye Yanga wamempandisha na kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Katika mahojiano yake ya kwanza na chombo cha habari nchini alipozungumza na blog ya SALEHJEMBE, alisema wachezaji kukaa nje kwa mapumziko kwa wiki mbili, si sawa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV