November 14, 2016

                                                                                                                                                                              
                       
MISS Ilala mwaka huu, Julitha Kabete amekula shavu baada ya kushinda vigezo vya kuiwakilisha Tanzania katika kinyang’anyiro cha mashindano ya Afrika yatakayofanyika Novemba 28, mwaka huu nchini Nigeria.
Julitha mwenye miaka 19, ndiye aliwabwaga kwenye kiti cha ulimbwende wa Wilaya ya Ilala mwaka huu kabla ya kuwabwaga tena kwenye Miss Dar City Centre, lakini akaanguka katika kiti cha ulimbwende wa Taifa lakini akifanikiwa kuingia kwenye Tano Bora.

Mashindano hayo yajulikanayo kama Miss Afrcia 2016 ni mara yake ya kwanza kufanyika, yenye lengo la kuibua vipaji vya mabinti kati ya miaka 18-27 kwa ajili ya kuwatumia kama mabalozi wa kutangaza suala zima la uchumi na mazingira kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika.

Mrembo huyo anayetokea kwenye kampuni ya Millen Magese Group amepewa Baraka zote leo Jumatatu na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kumkabidhi bendera ya taifa katika uwakilishi wake.
Aidha mshindi wa kwanza kwenye mashindano hayo, atajinyakulia kitita cha dola 35,000 pamoja na ndinga mpya, mshindi wa pili ataondoka  na dola 25,000 huku mshindi wa tatu akijipatia kitita cha dola 10,000.
Aidha waziri Nape alisema: “Tunataka mashindano ya Miss Tanzania ambaye anafaidika siyo mshindi peke yake tumeona hapa huyu alikuwa mtu wa nne na amepata nafasi ya kuwakilisha nchi, tunafahamu mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi vizuri na tutaendelea kuyaimarisha yawe bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri na siku moja hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania.”


Julitha ni nani?
Ni binti aliyezaliwa miaka 19 iliyopita jijini Dar es Salaam, kielimu ni mhitimu wa elimu ya upili (A-Level) nchini Afrika Kusini ambapo alichukua masomo ya Uchumi, Biashara na Ubinifu.
Mwaka huu amefanikiwa kutwaa mataji mawili kwa mpigo; Miss Ilala na Miss Dar City Centre.
Tayari amekuwa akijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa vitabu kwa watoto mashuleni pamoja na misaada mahospitalini. Aidha anajihusisha pia na ubinifu ‘fashion’ na ujasiriamali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic