November 14, 2016Beki Serge Wawa amerejea katika klabu yake ya zamani ya El Merreikh na kusaini miaka miwili.

Wawa raia wa Ivory Coast alijiunga na Azam FC akitokea katika klabu hiyo ya Sudan.

Lakini amerejea tena Sudan ikiwa ni siku chache baada ya kueleza kuwa Kocha Zeben Hernandez ambaye anainoa Azam FC kuonyesha hamtaki.


Wawa alikuwa kati ya beki tegemeo wa Azam FC, lakini alianza kuyumba na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya kuwa majeruhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV