November 15, 2016


Pamoja na kipigo cha mechi mbili mfululizo, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema kamwe hawatakurupuka katika usajili.

Omog amesema watakachofanya ni kuangalia kila wanachoona sahihi bila ya kuwa na papara.

"Kabla ya kufanya usajili, unaamua mambo mengi ya msingi. Kabla ya kumuacha mchezaji, kuna vitu vya kuangalia kabla ya kusajili tena.

"Hatuwezi kufanya usajili kwa hofu au haraka bila ya kujiridhisha nini tunataka. Tunajua namna ya kufanya," alisema Omog.

Simba imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ikiwa inaongoza kwa pointi mbili. Hii ni baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika mzunguko huo mwishoni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV