November 15, 2016
Kocha Hans van der Pluijm alikuwa mmoja wa makocha waliotakiwa na klabu ya Orlando Pirates na bado haijaacha kufanya hivyo.

Mmoja wa maofisa wa klabu hiyo, amesema Pirates ni klabu kubwa. Inapofikia inahitaji kufanya mabadiliko, huwa na namna ya aina yake.

"Kwanza tunatanua wigo na kuangalia mbali. Tunaangalia zaidi ya makocha sita au saba ili kupata uhakika," alisema Samson Jere.

"Pluijm ni kocha mzuri na kweli tulionyesha nia, lakini hatujaifuta," alisema.

Baada ya taarifa za Pluijm kuwa huru masuala hayo ya kutakiwa sehemu mbalimbali yaliibuka, ingawa taarifa nyingine zinaeleza Pirates iliwahi kumtaka Pluijm tokea akiwa anaendelea na kazi yake Yanga na hakukuwa na dalili za kuachwa.

Yanga imeingia mkataba na Kocha George Lwandamina raia wa Zambia ambaye anachukua nafasi ya Mholanzi huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV