November 20, 2016Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu yaani hat trick wakati Real Madrid ikiiangusha Atletico Madrid nyumbani kwake Vicente Calderon jijini Madrid na hiyo ikawa ni hat trick ya 39 katika maisha ya soka ya Ronaldo.


Lakini kitu kikubwa kabisa kwa kwa Ronaldo ni kwamba, amefanikiwa kuivuka rekodi ya gwiji la Madrid, Alfred di Stefano katika ufungaji wa mabao katika derby ya timu hizo kubwa za jiji la Madrid, pia nchini Hispania.


Di Stefano alikuwa amefunga mabao 17 wakati akiichezea Madrid dhidi ya Atletico lakini Ronaldo aliyekuwa anashika nafasi ya tatu, hat trick yake imemfanyah kufikisha mabao 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV