November 20, 2016


Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu amesema imekuwa bahati yeye kunusurika katika ajali ya gari iliyotokea jana.

“Kweli ni bahati tu, ajali ilikuwa mbaya sana kwa kweli,” alisema.

Hata hivyo Busungu hakutaka kuzungumzia zaidi kwa kuwa bado alikuwa katika harakati ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa baada ya ajali hiyo.

Jana, SALEHJEMBE ililazimika kufanga kazi ya ziada kupata taarifa za ajali hiyo baada ya kuenea kwa uzushi kwamba Busungu alipata ajali na kufariki dunia.


Taarifa zinaeleza alikuwa njiani kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ndipo alipokutana na masahibu hayo lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu alitoka salama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV