November 29, 2016
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilikutana jana Jumapili Novemba 27, 2016 kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia mashauri manane  na moja wapo ni ile ya Yanga iliyokuwa ikidaiwa na wachezaji wake wa zamani na kusisitizwa kuwalipa.

Shauri la 6. Malipo ya wachezaji Jerry Tegete, Omega Seme na Thabit Mohammed

Kamati iliamua utekelezwa ufanyike kwa Klabu ya Young Africans kuwalipa wachezaji hao kama uamuzi ulivyokwisha kutoka hapo awali. TFF iandikie barua Young Africans kuhakikisha inawalipa. 

Shauri la 7. Madai ya Mchezaji Said Bahanuzi dhidi ya Young Africans.

Suala la Bahanuzi limesogezwa mbele basi kwa kwa kuwa halikujadiliwa.

Shauri la 8. Mchezaji Said Hussein Morald


Mchezaji huyo kwa sasa ni huru baada ya yeye na Klabu ya Singida Unitedf kufikia mwafaka kwa barua ambazo waliwasilisha mbele ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV