November 22, 2016

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji aliungana na mamia ya waombelezaji waliojitokeza  kuuaga mwili wa aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Issack Shekiondo aliyeaga dunia Novemba 19 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Manji aliongozana na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga na baadhi ya viongozi wa Yanga kwenda kuuanga mwili wa kiongozi huyo wa zamani wa klabu hiyo ambaye aliagwa leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  (KKKT), lililopo Temeke na kusafirishwa Mkoani Tanga ambapo anatarajiwa kuzikwa leo katika kijiji cha Zege Kata ya Chindila Tarafa ya Bungu. 


Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa marehemu msemaji wa familia, Omlipa Chidi alisema kuwa, kabla ya marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari pamoja na presha ambapo kabla ya kufikwa na umauti alizidiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Amana kisha kukimbizwa katika hospitali ya Muhimbili ambapo mauti yalimfika Novemba 19 .


Aidha aliongeza kwa kusema kuwa, marehemu ameacha mke mmoja anayeitwa na watoto wanne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV