![]() |
| MMILIKI WA BLOG YA SALEHJEMBE, MWANDISHI MAHIRI WA MICHEZO NCHINI TANZANIA, SALEH ALLY AKIWA NA MWANDISHI MAHIRI WA MASUALA YA BURUDANI PIA KIJAMII, MILLARD AYO. |
Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC, limeitaja Blog ya Salehjembe ndiyo iliyotafutwa zaidi kuliko nyingike zote za michezo mtandaoni.
BBC kupitia mtandao wake wa Kiswahili, imeeleza Salehjembe imeshika nafasi ya nne kusomwa au kutafutwa zaidi kupitia mtandao namba moja duniani wa Google.
BBC imesema, Salehjembe imetafutwa au kusomwa zaidi kwa Tanzania kwa mwaka 2016 baada ya wale waliotafuta matokeo ya darasa la saba.
Namba mbili imekwenda kwa mtandao wa burudani wa Beka Boy, tatu ni mtandao wa kamari wa Mkeka Bet na mtandao wa michezo ni Salehjembe ulioshika nafasi ya nne.
Hivyo kama utasema mtandao wa habari, maana yake Beka Boy imeingoza na kufuatiwa na Salehjembe kwa mujibu wa Google na taarifa yake kuandikwa na BBC.
Mambo yaliyotafutwa sana Tanzania 2016:
1. Matokeo ya darasa la saba 2016
2. Beka boy
3. Mkekabet
4. Salehjembe juni 26 2016
5. Malazi Arusha
6. Euro 2016
7. Matokeo ya kidato cha nne 2016
8. Yinga media
9. Muungwana
10. Raymond








Hongera sana, me ni mmoja Kati ya wasomaji wa blog hii, habari za uhakika na wa wakati bila upended
ReplyDeleteupendeleo