December 18, 2016


Mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel Martin amesema bado ana nafasi ya kupata namba katika kikosi cha kwanza lakini amekiri haitakuwa kazi rahisi.

Martin amesema anaamini Yanga ina kikosi kipana na chenye ushindani.

“Kikosi cha Yanga si mchezo, kuna kazi ngumu kupata nafasi ya kuanza. Lakini naamini katika suala la juhudi.

“Nitashirikiana na wenzangu ili niwe sehemu ya msaada wa timu. Inaweza kuchukua muda lakini sitakata tamaa,” alisema.

Martin amesajiliwa na Yanga akitokea katika kikosi cha JKU ya Zanzibar.


Alisajiliwa baada ya kuifungia JKU bao moja wakati iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya kirafiki wiki iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic