|
Mhasibu wa Hawaii Products Suppliers, Said Ali Khamis (kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Luteni Kanali, Charles Mbuge baada ya pande zote mbili kusaini mkataba huo, leo.
|
Kampuni hiyo ambayo inasambaza maziwa ya Cowbell, itaidhamini Ruvu kwa mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Mwenyekiti wa Ruvu Shooting, Kanali Charles Mbuge, alisema: “Tunaishukuru kampuni hii kwa hiki walichokifanya kwetu, awali tuliomba udhamini kwa makampuni mengi lakini hatukufanikiwa.”
Naye meneja masoko wa kampuni hiyo, Elisaria Ndeta, alisema; “Lengo la udhamini wetu huu ni kuona tunainua mchezo wa soka hapa nchini kwa sababu timu zikiwa na udhamini zinakuwa na hali nzuri kiuchumi na kuifanya kushiriki vema, tunaomba makampuni mengine yafanye kama hivi.”
Katika pesa hizo, Sh milioni 15 wamekabidhiwa mkononi huku zilizosalia zikitumika katika kununulia vifaa kama mipira, koni na vitu vingine vya umuhimu kwa timu hiyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment