December 16, 2016



Katika hali isiyotarajiwa, jana Alhamisi mashabiki wa Yanga walioungana na wa Simba, kwa pamoja kuipokea timu ya Simba ilipowasili mkoani Lindi ilipokuwa inaelekea Mtwara kucheza dhidi ya Ndanda.

Simba ambayo keshokutwa Jumapili itapambana na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, ilifika Lindi na kupata fursa ya kufungua Tawi la Simba Kwanza Kitomanga lililopo mkoani hapo.


Mwenyekiti wa tawi hilo, Remy Mohammed Mpamba, amesema kuwa: “Kikosi cha Simba kilifika hapa saa 9:15 alasiri na kilikaa kwa saa moja kabla ya kuendelea na safari ambapo tulipata fursa ya kupiga nao picha huku Kocha Joseph Omog akikata utepe wa kufungua tawi letu.

“Kitu kizuri ambacho kila mmoja amekipenda hapa ni kwamba, watani zetu wa jadi, Yanga, tulishirikiana nao kwa kila kitu na wote tulikuwa wenye furaha huku tukiweka pembeni tofauti zetu.

Aidha, Mpamba alisema waliwazawadia Simba nyama ya mbuzi pamoja na fedha kidogo za kujikimu huku akiwataja Shiza Kichuya, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Laudit Mavugo na Jamal Mnyate kuwa ndiyo walikuwa gumzo kutokana na kila shabiki kutaka kupiga nao picha.



Aliongeza kuwa, wakati gari la Simba likitaka kuondoka eneo hilo, mashabiki wa Simba na Yanga, waliomba lisiwashwe na badala yake wakaanza kulisukuma kwa umbali wa zaidi ya kilomita tano.

1 COMMENTS:

  1. safi sana wana Yanga Lindi, kwenye soka hakuna rafiki wala adui wa kudumu, kesho simba itaomba yanga ishinde ili simba ipate nafasi ya ubingwa and virse versa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic