Klabu ya Azam, imetangaza kuwa, aliyekuwa kiungo wao mshambuliaji, Farid Mussa, Januari, mwakani anatarajiwa kujiunga rasmi na Tenerife ya Hispania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.
Farid ambaye alitakiwa kujiunga na timu hiyo Agosti, mwaka huu baada ya kufuzu majaribio, alishindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa kibali cha kufanyia kazi nchini humo ambapo tayari amekipata.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd amesema: “Tunashukuru safari ya Farid imeiva na rasmi Januari atajiunga na timu yake hiyo mpya kwani tayari vibali vyote vimekamilika kuanzia visa mpaka kibali cha kufanyia kazi.
“Muda wowote kuanzia leo ataondoka nchini kwenye Hispania kuanza maisha yake mapya, tunamtakia kila la heri huko aendako.”
Naye Farid alisema: “Nashukuru Mungu kila kitu kimeenda sawa, nitajiunga na timu yangu mpya Januari, ni jambo jema kwangu kwani ni kwa muda mrefu nilikuwa nahangaikia kitu hicho tu, lakini sasa hivi kimepatikana.”








0 COMMENTS:
Post a Comment