December 17, 2016



Mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel Martin, ameweka wazi kuwa anafurahia kupewa jezi iliyokuwa ikivaliwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Frank Domayo ‘Chumvi’ aliyeondoka kikosini humo mwaka 2014.

Martin aliyejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea JKU ya Zanzibar, ameanza kuvaa jezi namba 18 juzi Alhamisi alipoanza rasmi mazoezi na kikosi hicho baada ya kuingia kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo. 

Martin alisema: “Wakati naenda kukabidhiwa jezi, chaguo langu lilikuwa ni namba 19, ambayo nilikuwa nikivaa JKU, hivyo kwa bahati mbaya hapa nimekuta anaivaa Geoffrey Mwashiuya, hivyo sikuwa na namna kwani tayari zilikuwa zimebaki jezi mbili tu ambazo ni namba 18 na 2.

Martin ametua Yanga hatua za mwisho kabisa baada ya Yanga kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU na kuchapwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, yeye akiwa amefunga bao moja na kuipa shida safu ya ulinzi ya Yanga.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic