Huku ikionyesha soka safi la kitabuni utadhani Barcelona ya Hispamnia, timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa FC) imeishushia kipigo cha mabao 3-0 Gymkhana.
Taswa iliifunga Gymkhana katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Viwanja vya Gymkhana, Posta jijini Dar es Salaam.
Gymkhana waliokuwa nyumbani, walilazimika muda mwingi kuutafuta mpira kwa tochi, licha ya kuwa na mwanga wa kutosha uwanjani hapo.
Katika mechi hiyo, iliyojaa na ubabe mkubwa Taswa walipata bao lao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao, Julius Kihampa alilolifunga katika dakika ya tano ya mchezo akipokea pasi ya Ally Mkongwe.
Mabao hayo mazuri ya Kihampa na Mbozi 'Mchina' aliyefunga mawili, yalionyesha kuwaudhi Gymkhana ambao walipoteana na kuanza ubabe.
Taswa walipata bao la pili katika dakika 65 za mchezo huo kupitia kwa kiungo wake mkabaji, Mbozi Katala kabla ya kuongeza la tatu dakika 70 ya mchezo huo.
Wakati mechi hiyo ikiendelea, dakika ya 78, Gymkhana wakiongozwa na Juma Pinto walionekana kubadilika kwa kulishambulia goli la Taswa, lakini uimara wa safu ya ulinzi ya timu ilijatihidi kuokoa hatari golini kwao.
Baada ya mechi hiyo, Gymkhana walilazimika kufanya kikao huku baadhi wakiomba Taswa FC wasialikwe tena, ingawa hawakusema ni kutokana na pasi nyingi walizopigiwa au mabao mengi waliyofungwa kwenye uwanja wa nyumbani kwao ambalo kwao si jambo la kawaida.








0 COMMENTS:
Post a Comment