December 18, 2016


FULL TIME:
 
Mwamuzi anamaliza mchezo, Simba wanaondoka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
 
Dakika ya 90 + 3: Mchezo bado unaendelea na mpira unachezw akatikati ya uwanja muda mwingi.
 
Dakika ya 90 + 3: Mwamuzi anaweza kumaliza mpira muda wowote kuanzia sasa.
 
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

 Dakika ya 85: Simba sasa wanacheza kwa kujiamini zaidi baada ya kujihakikishia ushindi zikiwa zimesalia dakika chake.
 
Dakika ya 81: Mohamed Ibrahim anaipatia Simba bao la pili baada ya mpira kumgonga beki wa Ndanda na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.
 
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
 
Dakika ya 78: Simba wanafanya shambulizi kali, Kichuya anapata nafasi ya kupiga shuti ndani ya eneo la Ndanda, anapiga lakini beki wa Ndanda anaweka mguu na mpira unatoka nje kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
 
Dakika ya 77: Ndanda wanafanya mabadiliko, Omary Mponda anatoka nafasi yake inachukuliwa na Lukindo lakini wakati Mponda anatoka alionyesha kutofurahishwa na kutolewa, alitoka bila kumsemesha mwingine yeyote mopaka kwenye benchi.
 
Dakika ya 70: Simba wanapambana kutafuta bao la pili, wanaongeza kasi ya mashambulizi kwenye lango la Ndanda.
 
Dakika ya 63: Simba wanapata bao kupitia kwa kiungo wao, Mzamiru ambaye alipiga shuti ndani ya eneo la 18 likajaa wavuni ikiwa ni baada ya kazi nzuri ya Mohamed Ibrahim aliyewachambua walinzi wa Ndanda.
 
Goooooooooooo MZAMIRUUUUUUU

Dakika ya 59: Simba wanapata nafasi ya wazi wanashindwa kuitumia, Mohamed Ibrahim anaingia na mpira, anapiga krosi lakini Kichuya anapiga shuti jepesi akwa uso kwa uso na kipa wa Ndanda na shuti lake linadakwa.
 
Dakika ya 50: Matokeo bado ni 0-0, Ndanda wanaonekana kujipanga na kuwa wagumu kufungika licha ya Simba kupiga pasi kadhaa za kutafuta upenyo.
 
Dakika ya 52: Simba wanapata kona, inapigwa lakini wanashindwa kuitumia vizuri, walinzi wa Ndanda wanaondoa mpira.
 
Dakika ya 47: Timu zote bado zinasomana na mchezo umeanza kwa kasi ya taratibu.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO
Dk 45+3, Ndanda wanaingia vizuri tena, kwoshi ya Kiggi, lakini Agyei tena anatokea na kudaka
Dk 45+2 Ndanda wanaingia vizuri kabisa tena, wanapata kona, inachongwa na Kiggi, Agyei anapangua na mabeki Simba wanaondosha
DK 45+1 Ndanda wanapoteza nafasi nzuri kabisa mabeki wa Simba wakiwa wamejisahau

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 45, Ajibu anapiga vizuri kabisa lakini ni goal kick
DK 44, Simba inapata faulo baada ya Mo Ibrahim kuangushwa na Mtama. Si mbali.
Dk 40, Simba wanapata nafasi nyingine, lakini Mo Ibrahim anashindwa kupiga shuti vizuri baada ya mpira kudunda kwenye uwanja
Dk 36, Simba wanapata nafasi nyingine lakini Ajibu anachonga krosi fupi, Ndanda FC wanawahi

Dk 35 sasa, Simba wanaonekana kuimarika katika  nafasi ya kiungo. Hata hivyo bado hakuna mashambulizi makali huku ndanda wakionekana kupunguza mashambulizi tofauti na walivyoanza
Dk 33, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa vizuri, Blagnon anaruka na kupiga kichwa. Kipa anadaka kwa ulaini
Dk 27, Ajibu anaingia na kupiga shuti kali, linamgonga beki wa Ndanda na kuwa konalakini haina faida
Dk 24, Ndanda wanaingia vizuri tena, Mponda anapijga shuti kali lakini linaishia mikononi mwa Agyei

Dk 22, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini Bokungu anatoa na kuwa kona. Inachongwa na Kiggi, haina faida
Dk 18 sasa mpira bado hauna ladha sana na mashambulizi bado si makali
SUB Dk 15 Yassin Muzamiru anaingia kuchukua nafasi ya Kotei ambaye anaonekana ameumia baada ya kugongwa kiwiko na Kiggi
Dk 13, Mpira umesimama hapa baada ya kiungo wa Simba Kotei kugongwa kiwiko wakati akigombea mpira na Kiggi Makasi
Dk 11, Agyei analazimika kufanya kazi ya ziada kupambana na mshambuliaji wa Ndanda ili kumpokonya mpira, tayari alishamtoka Mwanjale

Dk 6, krosi nzuri ya Kigi Makasi lakini AAgyei anatoka na kudaka vizuri
Dk 3, krosi safi ya Kichuya, inamfikia Blagnon anapiga kichwa lakini anashindwa kulenga lango
Dk 2, Ndanda wanaingia tena hapa, Paul Ngalema anajaribu lakini Agyei anaudaka na kuanguka
Dk 1, Ndanda wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Simba, anapiga shuti kali hapa Hamisi Rifat lakini hakulenga lango



KIKOSI CHA SIMBA
1. Daniel Agyei
2. Bosaka Bukungu
3. Mohamed Zimbwe 
4. Method Mwanjale
5. Abdi Banda
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. James Kotei
9. Frederic Blagnon
10 Ibrahim Ajibu
11. Mohamed Ibrahim 

Benchi
Peter Manyika
Hamad Juma
Said Ndemla
Laudit Mavugo
Jamal Mnyate
Novaty Lufunga
Mzamiru Yassin

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic