December 19, 2016



Kocha Mkuu wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ raia wa Croatia, ameibuka na kusema kuwa bado anaipenda Tanzania, hivyo anatamani siku moja arudi kufundisha moja kati ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

Loga ambaye alijiunga na Simba Desemba, 2013 na kupewa mkataba wa miezi sita uliomalizika mwishoni mwa msimu wa 2013/14 kabla ya kuongezewa mwaka mmoja, kwa bahati mbaya hakumaliza mkataba wake huo mpya, akatimuliwa baada ya kuutumikia kwa takriban wiki tatu kwa kile kilichoelezwa ni kutofautiana na viongozi wake.

Kocha huyo ambaye hivi karibuni amemaliza mkataba wake wa kuinoa Interclube ya Angola, siku chache kabla ya mkataba wake huo kumalizika, alifanikiwa kuiongoza kubeba ubingwa wa kombe la chama cha soka cha nchi hiyo (APFL) baada ya kuinyuka Petrol mabao 3-0.

“Kwa sasa nipo Croatia baada ya mkataba wangu kumalizika kule Angola, sina timu na nafanya mpango wa kupata sehemu nyingine ya kufundisha, matarajio yangu makubwa ni kuja tena Tanzania kufundisha, kwani bado napapenda.


“Nimeachana na Interclube baada ya kuinoa kwa siku 284 na kucheza mechi 39 nikiwa kama kocha mkuu, sina budi kuwashukuru Waangola kutokana na ushirikiano walionipa kwa wakati wote niliokuwa kwao,” alisema Loga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic