December 18, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amewapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT lakini akasisitiza, wanatakiwa kufanya kazi zaidi.

Lwandamina amesema vijana wake walicheza vizuri katika kipindi cha pili, lakini bado hajaridhika.

“Bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia tunachotaka. Soka ni mchezo unaobadili mambo kila wakati kulingana na yanayotokea uwanjani,” alisema.

“Tutarudi mazoezini na kurekebisha mambo kadhaa ambayo yanaweza kutusaidia kufanya vizuri zaidi kwa kuwa safari bado ni ndefu na tuna mechi nyingi mbele.”

Lwandamina amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm ambaye sasa ni mkurugenzi wa ufundi.

Ushindi wake wake dhidi ya JKT unamfanya awe ameanza ligi vizuri na anaonekana amepania kuendeleza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic