January 25, 2017Kiungo wa Yanga anayefanya vizuri hivi sasa akiwa na kikosi cha timu hiyo, Simon Msuva huenda akatimka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake baada ya kiungo wa zamani wa Yanga, Credo Mwaipopo kumtaka amfuate Ulaya.

 Msuva amebakiza mwaka mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wake wa kuitumikia Yanga.

Credo ambaye anafanya shughuli zake nchini Sweden amesema kwa kiwango cha mchezaji huyo anatakiwa kuondoka hapa nchini na kwenda nchini humu kwani uwezo wake ni mkubwa.

Mwaipopo, alisema kuwa kutokana na uwezo wa juu wa kucheza soka alionao hivi sasa Msuva hastahili kuendelea kucheza Ligi Kuu Bara bali akajaribu bahati yake ya Ulaya.


“Nimekuwa nikifuatilia Ligi Kuu Bara na Msuva ni mmoja kati ya wachezaji ambao wanafanya vizuri, nimekuwa nikiwasiliana naye muda mrefu na kumwambia kuwa hatikiwi hivi sasa kuwa hapa nchini kutokana na uwezo wake.


“Soka hivi sasa linalipa na kwa uwezo wake alionao hastahili kuwa hapo na ukizingatia umri wake bado mdogo ambao ndiyo unaohitajika zaidi Ulaya, Watanzania wengi tumeshindwa kufanya vizuri huko kutokana na kuchelewa kutoka nchini hivyo tulipofika huko tayari umri ulikuwa umeshatutupa mkono.


“Naamini kabisa Yanga ni waelewa watamruhusu aondoke akajaribu bahati yake katika kipindi hiki ambacho bado umri wake unamruhusu na sisi tupo huko tunajua jinsi gani ya kumsaidia akishakwenda Sweden.

“Nafikiri huyu ni Mtanzania na sisi kama Watanzania ni jukumu letu kumsaidia,” alisema Mwaipopo.

Alipoulizwa Msuva kuhusiana na suala  hilo alisema: Ushari wake huo nimeusikia ni mzuri na ameutoa muda mzuri ambao na mimi nilikuwa na ndoto za kwenda huko mara tu baada ya kumalizika kwa mkataba wangu na Yanga.”


Msuva ambaye amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha Yanga kwa sasa ana mabao tisa sawa na kinara Shiza Kichuya kwenye Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV