January 25, 2017



Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ametamba kwamba hatishwi na hali ya wapinzani wao Yanga kuwakaribia kileleni kwani kikosi chake bado kinaongoza kwenye ligi.

Omog mpaka sasa ameisaidia Simba kukwea kileleni mwa ligi wakiwa na pointi 45 mbele kwa pointi mbili ya mahasimu zao Yanga ambao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 43.


Kocha huyo wa zamani wa Azam amesema kwamba kwake hatishwi na hali ya kukaribiwa na Yanga katika mbio za kuwania ubingwa kwa sababu bado kikosi chake kipo mbele na kinaongoza ligi.


“Hatutishwi na Yanga kusogea karibu yetu badala yake ndiyo wanatupa hali ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo ili tuweze kuwakwepa na mwishowe tuweze kutwaa ubingwa.


“Wanachotakiwa kutambua kwamba sisi tuko mbele yao na mikakati yetu ni kuona hatuondoki kwenye nafasi hiyo mpaka mwisho wa msimu lakini tunatakiwa kuongeza juhudi zaidi kwenye mechi zetu zinazokuja kwa kupata ushindi,”alisema Omog.

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic