January 29, 2017


Senegal iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Afcon, imetolewa katika hatua ya robo fainali na Simba Wasioshindika, Cameroon wamesonga mbele.

Cameroon wamesonga mbele baada ya ushindi wa penalti 5-4, penalti ya mwisho ya Senegal ilipotelea kwa nyota wake Sadio Mane anayekipiga katika kikosi cha Liverpool nchini England.


Kwa Liverpool itakuwa furaha kuu maana bila Sane mambo yalionekana yanakwenda kombo. Lakini kwa Wasenegali ni majonzi makubwa wakiwa wanaenda nyumbani.

Katika mechi hiyo, dakika 90 halafu 120 ziliisha kwa sare ya bila mabao huku Senegal ikiwa imepoteza nafasi nyingi za kufunga.

 PENALTI ZILIVYOKUWA
SENEGAL
Koulibaly - FUNGA
Kara - FUNGA
Sow -FUNGA
Saivet - FUNGA
Mane - KOSA 


CAMEROON
Moukandjo - FUNGA
Oyongo - FUNGA
Teikeu - FUNGA
Zoua - FUNGA
Aboubakar - FUNGA






Senegal (4-3-3): Diallo; Gassama, Kara, Koulibaly, M'Bengue (Ciss 86mins); Gueye, Saivet, Kouyate (Ndiaye 109); Mane, Diouf (Sow 64), Keita.
Booked: Diouf, Kouyate.


Cameroon (4-3-3): Ondoa; Fai, Teikeu, Ngadeu-Ngadjui, Oyongo; Siani, Moukandjo, Djoum (Mandjeck 102); Bassogog, Tambe (Aboubakar 102), Ekambi (Zoua 46).

Booked: Oynogo, Fai, Djoum.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic