January 29, 2017


Lionel Messi ameonyesha fedha si chochote kwa mzazi, maana amenunua chupa mvili za mvinyo kila moja ikiwa na thamani ya pauni 430 (zaidi ya Sh milioni 1.3).

Maana yake kwa chula mbili ni Sh milioni 2.6 ikiwa ni kukamilisha sherehe ya miaka 57 ya mama yake mzazi airway Celia.

Mvinyo huo ghali aina ya Vega-Sicilia's Unico, ulionekana kwenye picha za mtandao wa Instagram wakati Messi akisherekea pamoja na mama yake.

Baadaye alitupia picha wakati Celia akiwa anasherekea na wajukuu zake.


Messi ni raia wa Argentina ambaye alihamia Hispania akiongozana na baba yake, wakati huo Messi akiwa na umri wa miaka 13.


Messi alitua Argentina akiwa amekwenda kutibiwa ugonjwa wa kukua huku akitakiwa kujiunga na Barcelona ambayo aliiomba imsadie gharama za matibabu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic