January 16, 2017

Kiungo wa Simba, Mohamed Ibrahim ataokosa mechi kati ya timu yake mpya dhidi ya ile ya zamani.

Kikosi cha Simba kiko tayari kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, keshokutwa.

Mo Ibrahim aliumia kifundo cha mguu katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi.


Lakini tayari ameanza mazoezi ya taratibu huku akiendelea na vipimo.
Imeelezwa, jana alifanyiwa vipimo na amekuwa akiendelea na matibabu.

Pamoja na kumkosa Mo Ibra, Simba ina wachezaji wengi wanaoweza kuziba pengo lake kwa kuwa amekuwa chaguo namba moja la Kocha Joseph Omog.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV