January 15, 2017

SIMBU (KATIKATI) MARA BAADA YA KUSHINDA MARATHONI YA MUMBAI, LEO. WENGINE NI WAKENYA, JOSHUA KIPKORIR NA ELIUD BARNGETUNY WALIOSHIKA NAFASI YA PILI NA TATU.

Felix Simbu ameshinda Mumbai Marathoni na kufanikiwa kupata zawadi ya medali ya dhahabu na fedha taslimu dola 67,000 (Sh milioni 149).

Katika mbio hizo ambazo ni moja ya zile maarufu duniani, Simbu alitumia muda wa 2:09:32
hadi alipomaliza, leo.


Mkenya Joshua Kipkorir ndiye alishika nafasi ya pili akiwa amemaliza kwa tofauti ya sekunde 18 na Simbu.

Mkenya mwingine, Eluid Barngetuny naye alimaliza katika nafasi ya tatu hivyo kumfanya Simbu kuwa kiboko ya Wakenya ambao wanasifika kwa mbio hizo ndefu.


Katika hatua za mwisho  Chesari, Bonsa Dida na Simbu ndiyo walichuana vikali. Hata hivyo zikiwa zimebaki kilomita tano, taratibu Bonsa alionekana kuchoka na kuwaacha Simbu na Chesari wakiendelea kuchuana vikali.

Kama unakumbuka Simbu anayedhaminiwa na Multichoice Tanzania baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kumuombea, alionyesha uwezo mkubwa tokea mwanzo wa mbio hizo za Mumbai nchini India.


Simbu amewashinda Wakenya na Waethiopia na sasa anapata nafasi ya kushiriki michuano ya ubingwa wa dunia pamoja na London Marathoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic