January 9, 2017Pamoja na kukosa mabao mawili ya wazi, kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amefunguka kuwa bado walikuwa wana uwezo wa kufunga mabao mengine matatu katika mchezo wa juzi Jumamosi dhidi ya Yanga kutokana morali waliyokuwa nayo.

 Azam ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar na kuwafanya kuongoza Kundi B wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Yanga wenye sita.

Sure Boy amesema kuwa siri kubwa iliyosababisha waibuke na ushindi huo wa kihistoria ni kutokana na kujiamini zaidi licha ya kupewa nafasi finyu huku akisisitiza kuwa walikuwa wana uwezo wa kufunga mabao mengine matatu kama muda ungeongezwa zaidi.

“Unajua siri ya matokeo ya ushindi ni mipango ya mwalimu mpya ambaye tupo naye kwa sababu awali kocha ambaye ameondoka alikuwa na mipango yake huenda ilichangia timu kushindwa kucheza lakini mwalimu alituambia umuhimu wa mchezo wa leo (juzi), ndiyo maana tumefanikiwa kupata matokeo ambayo yameshangaza watu wengi kwa kuwa hatukuwa katika wakati mzuri hapo awali.


“Yanga ni timu  mkubwa ambayo tunaiheshimu siku zote lakini malengo yetu ilikuwa ni kuwafunga na tumeweza kufanya hivyo, maana naamini kama muda ungekuwa bado mwingi zaidi kipindi cha pili basi tulikuwa na nafasi ya kufunga mabao mengine matatu kwa kuwa morali yetu ilikuwa juu zaidi ya wapinzani wetu,” alisema Sure Boy.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV