February 19, 2017Simba wanaonekana wamepania kufanya kwenye katika mechi ijayo dhidi ya watani wao Yanga.

Katika kambi ya Simba mjini Zanzibar, kila kitu kinaonekana kuwa siri na hawataki kukizungumzia chochote.

Badala yake inaonekana kila kitu kinakwenda kwa ukimya kama watu waliopania kummaliza mpinzani kimyakimya.

Katika mechi ya kwanza katika Ligi Kuu Bara, Simba ililazimika kusawazisha kwa bao la Shiza Kichuya dakika za mwisho.

Hivyo Simba, wameamua kufanya maandalizi ya uhakika ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV