February 19, 2017Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameendelea kubaki hospitali kwa matibabu.


Hadi leo mchana, Manji ameendelea kuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa wasaidizi wa Manji ameiambia SALEHJEMBE, Manji bado anapata matibabu ya moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ndani ya Muhimbili.


“Kweli bado anapatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi,” alisema.


“Analindwa na askari sita hivi, wako wale wa kawaida na wa uahamiaji,” alisema.

Baada ya kupata dhamana katika kesi ya tuhuma za kutumia madawa ya kulevya, sasa Manji yuko chini ya ulinzi wa Uhamiaji.

Bado haijajulikana hasa anachotuhumiwa, lakini leo imeelezwa hali yake kuwa na nafuu lakini amekuwa akionekana ni mchovu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV