SINGO (MWENYE MIWANI), AKIZUNGUMZA MBELE YA MAOFISA WA TFF NA BODI YA LIGI |
Serikali imetoa wito na kuweka msisitizo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kuhakikisha wanamuweka mwamuzi sahihi kuamua mechi ya watani Simba na Yanga.
Mechi hiyo inachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Michezo,Yusuph Omary Singo amesema mwamuzi bora atapunguza kutokea kwa masuala ya jaza.
“Lazima muweke mwamuzi mwenye vigezo ili kuepusha haya mambo ya jazba ambayo yamekuwa yakijitokeza kila mara.
“Lakini mashabiki nao lazima wajue kwamba viti si sehemu ya mchezo. Tunawasisitiza kuwa wastaarabu na kwa wale ambao hawataelewa, sheria itachukua mkono wake,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment