February 20, 2017


Kwa wale wanaokwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kufanya vurugu hasa wakati wa mechi ya watani, Yanga na Simba itakaypigwa Jumamosi ijayo, waahirishe.



Kitengo cha ulinzi uwanjani hapo kimesisitiza kutakuwa na ulinzi mkali pamoja na kamera za ulinzi ambazo ziko tayari kwa kazi.

Hashim Abdallah ambaye ni mwamuzi lakini ni askari Polisi, amesisitiza wako imara na kuwaonya weote ambao wanafikiri wanaweza kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kung’oa viti bila ya kujulikana.



Kamera za kisasa zitatumika kuwanasa kila watakaofanya vurugu na mara moja hatua za kisheria zitachukuliwa.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyowakutanisha watani hao, mashabiki wa Simba wenye jazba waling'oa na kuvunja kiti hasa baada ya Amissi Tambwe kufunga bao upande wa Yanga. Kabla ya kufunga alishika, lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote na mashabiki hao wakaamua kumaliza hasira zao kwenye viti.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic