February 18, 2017


Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns wamefanikiwa kubeba ubingwa wa Super Cup baada ya kuichapa TP Mazembe kwa bao 1-0.

Mechi ya fainali ya Super Cup huwakutanisha mabingwa wa Afrika na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao safari hii ni TP Mazembe.

Sundowns ya Afrika Kusini ikiwa kwenye ardhi ya nyumbani jijini Pretoria ilipata bao lake kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 83.

Hata hivyo, wenyeji ndiyo walitawala mpira kwa muda mwingi zaidi kuliko TP Mazembe walionekana kujilinda zaidi.


Katika kipindi cha kwanza Mazembe walipoteza nafasi nzuri huku mpira ukigonga mwamba mara mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic