February 22, 2017
Video Queen wa Muziki wa Bongo Fleva nchini,  Agnes Gerald ‘Masogange’ leo Jumatano amefanikiwa kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota rumande kwa  zaidi ya wiki moja kufuatia kukamatwa kwa tuhuma za kutumia madawa za kulevya.

Masogange amefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka yake mawili ya kutumia madawa ya kulevya aina ya Narcotic na Oxazepam na wakili wa Serikali, Costantine Kalula ikiwa ni kinyume na sheria ya kupambana na madawa ya kulevya  ya mwaka 2016 kifungu 18 , kifungu kidogo A kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu mbele ya hakimu, Wilbroad  Mashauri.

Hata hivyo, mshatakiwa alikana makosa yote mawili ya kesi hiyo ambapo mawakili wake wa utetezi,  Reuben  Simwanza akaomba dhamana yenye masharti nafuu kwa teja wao ombi liliokuwa kubaliwa hakimu wa kesi hiyo.

Mashauri ametoa dhamana kwa video queen huyo  kwa kujitokeza wadhamini wa wawili ambao wamesaini bondi ya shilingi milioni 10 huku akitakiwa kutokutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kibali  maalum cha mahakama.

Kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Machi 21, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV