February 22, 2017


Wafanyakazi 14 wa Kampuni ya Quality Group waliokamatwa hivi karibuni wakihusishwa na kesi ya kufanya kazi nchini bila vibali vinavyowaruhusu kufanyia kazi leo wamefikishwa katika mahaka ya hakimu mkazi kiusutu leo na kusomewa mashataka yao.

Wafanyakazi hao wametajwa kwa majina ya Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamifu(29), Niradri Maiti (41), Divakar Raja(37), Mohamed Shailch(44),Bijenda Kumav(43), Pra soon Kumar(46), Nipun Bhalt(32).

Wengine wakiwa ni Pinto Kumar(28), Anuij Aggewa (46), Vanin Baloor (34), Avun Kateel(46), Auhash Chandratiwan(33) na Vikrain Sankohata (50), na kusomewa mashitaka matatu na Hakimu Sprian Mkeha, ambapo mashitaka yao yalitajwa  kubainika kuingia nchini kwa kugushi Visa na Kufanya kazi kinyume cha sheria za nchi kama washauri wa kampuni ya Quality Group na kujipatia kazi bila vibali kinyume na sheria za ajira kwa wageni.

Katika tukio hilo ambalo limemezua hisia kubwa kwa wadau huku likimhusisha pia Mshauri wa kampuni za Quality Yusuf Manji, Baada ya kusomewa mashitaka hayo kwa pamoja Watuhumiwa hao walikana kuhusika na tuhuma hizo, hivyo upande wa mashitaka ukaomba watuhumiwa wapelekwe rumande ili wapate muda wa kuendelea kukamilisha hatua za upelelezi wa kesi hiyo, ambapo upande wa mawakili watetezi wa kesi hiyo waliomba wateja wao wapatiwe dhamana muda wote wa kukamilisha ushahidi wa washitaki.

Watuhumiwa hao waliruhusiwa kudhaminiwa kwa masharti ya kila mmoja kuweka kiasi cha shilingi milioni tano huku watuhumiwa wakitakiwa  kujidhamini kwa kutoa kiasi hicho kwa kila mmoja, kesi hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na wakili wa Serikali, Method Kagome huku wakili wa washitakiwa Alex Mgongolwa, kwa pamoja waliridhia kesi hiyo kusikilizwa tena Machi 6 mwaka huu. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV