February 21, 2017Baada ya kuanza mazoezi, beki Method Mwanjale amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na daktari wa Simba kuhakikisha anakuwa fiti katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Yanga.


Mwanjale alikuwa majeruhi, lakini amerejea na kuanza mazoezi ingawa kila hatua imekuwa ikifuatiliwa na daktari huyo.


“Kwelia anafuatiliwa kwa karibu kabisa, kuna wakati alilazimika kubaki Dar atibiwe. Lakini imani yetu atarejea,” kilieleza chanzo.


Mwanjale ndiye beki tegemeo kwa upande wa Simba na amekuwa akiwaongoza mabeki wengine chipukizi iwe ni Abdi Banda au Novarty Lufunga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV