February 22, 2017
Ulanguzi wa tiketi za mechi baina ya watani wa jadi, Simba dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa, Jumamosi umeshika kasi kubwa.

Kinachoonekana kuna kundi la wafanyabiashara ambalo limejitokeza na kununua kwa wingi tikleti za Sh 7,000 na Sh 10,000 hali inayosababisha wengi kuhaha kuzitafuta,

Tiketi zimekuwa zikiuzwa kupitia MaxMalipo na ndani ya siku mbili tiketi 10,000 zilikuwa zimeuzwa lakini sasa inaonekana tiketi za bei ya chini zimeishaadimika wakati mechi ni Jumamosi.

Baadhi ya wadau wamelalamika hali ya kukosekana kwa tiketi hizo za bei ya chini jambo ambalo linaonekana kuwakwaza wengi.


Hata hivyo, inawezekana kabisa tiketi hizo zikaanza kuuzwa kwa kulanguliwa siku mbili au moja kabla ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV