February 22, 2017





Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji anaendelea kushikiliwa licha ya kutoa maelezo yake kwenye Ofisi za Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Ingawa kila kitu kimekuwa siri, lakini Manji jana alifika katika ofisi hizo uhamiaji na kutoa maelezo kwa zaidi ya saa mbili.

Baadaye magari yaliondoka na kuongozana hadi katika Hospitali ya Agakhan ambako ilielezwa anahamishiwa hapo.

Mmmoja wa wanasheria wanaosimamia kesi yake, Alex Mngongolwa alipopigiwa mara ya kwanza alisema apigiwe baadaye, ambapo alipopigwa alisema yuko hospitali alipigiwe tena baadaye.

Alipopigiwa mara ya tatu na kuulizwa kuhusiana na kipi hasa anachohojiwa Manji, alisema:

“Nilikuwa niko hospitali. Lakini kuhusiana anahojiwa au la, ni kuhusu wafanyakazi au vinginevyo, kweli siwezi kuzungumza kwa kuwa miiko ya kazi yangu inakataza. Labda mteja mwenyewe azungumze.”

Kabla, alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyo katika Hospitali Kuu ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kuanzia juzi, Manji alikuwa akilindwa na askari watano wakiwemo wawili wa uhamiaji. Jana, baada ya kuhojiwa waliongozana naye hadi katika hospitali ya Agakhan.

Hata hivyo, kumekuwa na ugumu wa kueleza Manji anaendelea kushikiliwa kwa suala lipi hasa la uhamiaji. Maana kuhusiana na tuhuma za kutumia madawa ya kulevya, aliishapata dhamana.

Kuhusiana na uhamiaji, haijajulikana ni suala la kudaiwa ana pasi mbili za kusafiria au lile la kampuni ya Quality Group kuajiri watu ambao hawakuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Juhudi za watu wa uhamiaji kuzungumzia suala hilo zilionekana kukwama kwa madai haujafikia wakati wa kulizungumzia.


SOURCE: CHAMPIONI (USIKOSE LIKO MTAANI LEO JUMATANO)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic