February 18, 2017

Yanga imefanikiwa kusonga mbele katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Ngaya Club ya Comoro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo Jumamosi.

Timu hizo zimetoka sare hiyo katika mchezo uliokuwa hauna presha kubwa kwa kuwa mchezo wa awali Yanga ilishinda kwa mabao 5-1 nchini Comoro.


 Katika mchezo uliochezwa Taifa, Wacomoro hao ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza mapema, kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa Haji Mwinyi katika dakika ya 43.

 
 

Katika mchezo huo wachezaji wa Yanga walipata nafasi kadhaa za wazi lakini wakashindwa kuzitumia vizuri, Obrey Chirwa alikosa bao katika dakika ya 48 na 51, Emmanuel Martin naye alishindwa kutumia nafasi ya wazi dakika y 56.

Kutokana na kushindwa kutumia nafasi alizopata, Kocha wa Yanga, George Lwandamina aliamua kumtoa uwanjani Martine na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Mahadhi ambaye naye alipata nafasi dakika ya 61 akashindwa kuitumia vizuri.

yanga ilifanya mabadiliko mengine kwa kumtoa Juma Abdul na kuingia Hassan Kessy dakika ya 71, Deus Kaseka naye akatoka dakika ya 81 na kuingiza Said Juma Makapu.

Kikosi cha Yanga kilichoanza katika mchezo huo ni
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Vicent Bossou
5. Kelvin Yondani
6. Justine Zulu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Obrey Chirwa
10. Deusi Kaseke
11. Emanuel Martin

Walioanzia benchi
- Ali Mustafa
- Hassani Kessy
- Oscar Joshua
- Vicent Andrew
- Nadir Haroub

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV