March 29, 2017Beki kisiki wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris jana jioni alianza rasmi mazoezi mepesi ya kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu washambuliaji wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe wapone majeraha ya goti na kuanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo.

Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana Aprili Mosi, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

Morris alisema anarejea uwanjani baada ya kupata nafuu ya majeraha yake ya mfupa wa paja la kulia wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland.

 “Namshukuru Mungu kwa kuweza kurejea uwanjani kwa sababu mchezaji lengo lake ni kucheza na siyo kukaa tu, hamna kitu kibaya kwa mchezaji kama kupata majeraha yatakayosababisha kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.


"Hivyo, hivi sasa nimepata nafuu ya majeraha yangu na kuanza mazoezi mepesi ya binafsi kabla ya kuanza programu ya mazoezi magumu na wenzangu katika kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga," alisema Morris.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV