March 29, 2017Baada ya Lionel Messi kufungiwa mechi nne na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kumshushia matusi mwamuzi wa pembeni, Klabu ya FC Barcelona imetoa tamko.


FC Barcelona imesema haiungi mkono waamuzi kunyanyaswa lakini adhabu ya Messi kwa timu yake ya taifa ni kubwa sana.


Uongozi wa Barcelona umesisitiza Fifa wametoa adhabu kubwa sana kwa Messi na walipaswa kumfikiria.

Messi alimtukana mwamuzi huyo wakati Argentina ilipocheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na kuifunga Chile kwa bao 1-0, yeye akiwa mfungaji.


Mechi iliyofuata, ikiwa ndiyo inamkosa Messi, Argentina ilitwangwa kwa mavao 2-0 na Bolivia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV