March 29, 2017Kiungo nyota wa Arsenal, Mesut Ozil ameonekana kuchoshwa na lawama za mashabiki wa Arsenal ambao ameamua kuwatolea uvivu.


Ozil raia wa Ujerumani, amesema anaamini amefanya vizuri katika soka kabla hajatua Arsenal na baada ya kutua katika kikosi hicho.

“Mafanikio yangu na Real Madrid kila mmoja anajua, mchezaji wa Ujerumani hadi Kombe la Dunia, inajulikana.

“Hapa Arsenal nilifunga mabao kadhaa, nikatoa pasi 20 zilizozaa mabao katika mechi zote. Sasa ajabu kabisa, timu ikifanya vibaya, ninawekwa pembeni na kupokea lawama zote.


“Kila ninapofanya vizuri inakuwa ni sisi, timu ikifanya vibaya ni mimi. Hii si sawa hata kidogo,” alisema akizungumza na kituo cha runinga cha ITV cha Uingereza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV